Msongo wa mawazo ni hisia ya kutoweza kukabiliana na mahitaji yanayotokana na kazi, mahusiano, shinikizo za kifedha, na hali zingine za maisha.
Ni kawaida kupata hisia za msongo wa mawazo, lakini isiposhughulikiwa,inaweza kuwa na madhara kwako. Inaweza kukufanya uwe lengo rahisi la magonjwa na hata kusababisha maswala ya afya ya akili kama vile unyogovu.
Tukio moja kuu maishani mwetu, janga la COVID-19, limekuja na changamoto ambazo wengi wetu hatujawahi kukabiliana nazo, na kusababisha msongo wa mawazo na wasiwasi zaidi. Hata kabla ya janga hilo, hali zingine za maisha kama mabadiliko ya maisha, maswala ya kazi / biashara, shinikizo za kifedha, mahusiano, na maswala ya kifamilia yalichangia sana kwa hisia za msongo wa mawazo na mafadhaiko.
Utajuaje iwapo wewe, ama mtu wa karibu wako ana msongo wa mawazo?
Sisi sote tunapitia msongo wa mawazo kwa njia tofauti. Mara nyingi, tunaweza kosa kujua kuwa tunachopitia ni msongo wa mawazo. Ikiwa unapata mabadiliko haya, kuna uwezekano kuwa unakabiliwa na msongo wa mawazo.
• Kupoteza hamu na tamaa ya kufanya uliyofurahiya hapo awali
• Kuhisi kushuka moyo, au kukosa tumaini
• Kuhisi vibaya kujihusu, au kuhisi kuwa umefelu maishani ama kwamba umeiangusha familia yako.
• Kujisikia uvivu au kuhisi kutotulia, kubabaika.
• Mawazo kwamba ungekuwa bora kufa au kujiumiza kwa njia fulani.
Je, unawezaje kudhibiti hisia za msongo wa mawazo?
Licha ya msongo wa mawazo kuwa kitu cha kawaida maishani mwetu, inaweza kuwa hatari isiposimamiwa vizuri.
Usiruhusu hisia zinazohusiana na mafadhaiko na msongo wa mawazo zidhibiti maisha yako. Ikiwa unahisi kusumbuka na kuzidiwa, unashauriwa kufanya:
1. Mazoezi
Shughuli kama vile kukimbia, kucheza mpira wa miguu, kutembea, na kucheza, kati ya
zingine zitasaidia kuinua mhemko wako na kukusaidia kulala vizuri. Kufanya mazoezi
mara kwa mara pia hukusaidia kusahau wasiwasi na shida zako na husaidia kusahau
mawazo ambayo yanasababisha msongo wa mawazo.
2. Kulala
Kulala hupunguza msongo wa mawazo sana. Kuwa na utaratibu wa kulala
husaidia kukutuliza, inaboresha hali yako na inakusaidia kufanya maamuzi bora.
Wataalamu wanapendekeza kulala kwa angalau masaa 8 kila usiku.
Jaribu kupata tabia bora za kulala kwa kufanya mazoezi, kupunguza unywaji wa
pombe au kafeini (chai / kahawa) wakati wa kulala unapokaribia.
3. Lishe Bora
Ingawa chakula hakiwezi kuondoa hisia za kuchanganyikiwa na msongo wa mawazo kabisa, lishe bora inaweza kuongeza mhemko wako, kupunguza shida za kuwa na shinikizo la damu, na kujenga kinga yako ya mwili. Kuna vyakula ambavyo vinaweza kupa utulivu wa msongo ikiwa unazijumuisha kwenye lishe yako ya kila siku. Hii ni pamoja na vyakula vyenye:
• Vitamini C na madini - matunda na mboga
• Protini kama mayai, nyama, na maharagwe.
• Vyakula vinavyotoa nishati kama mahindi, ngano na viazi vitamu.
4. Panga kazi yako na uorodheshe majukumu yako
Panga kazi zako za kila siku ukianza na kazi za haraka. Mwishoni mwa siku, zingatia majukumu ambayo umeweza kufanya. Hii itakusaidia kukumbana na hisia za kuzidiwa na shughuli zako za kila siku.
5. Wakati
Usibebwe sana na kasi ya maisha. Chukua muda kupumzika ili ufurahi na ufanye kitu unachofurahiya kila siku. Hii haitaongeza burudani zako tu, lakini pia itakupa kitu cha kutarajia.
6. Zungumza na watu unaowaamini
Kuzungumza na kuwaambia watu wa karibu nawe shida zako kunaweza kusaidia kupunguza viwango vyako vya msongo wa mawazo, huku kujumuika na familia na marafiki kukiweza kukusaidia kuwa mtulivu na kupunguza msongo wa mawazo. Ni vizuri kuzungumza na wengine kwani watu wanaweza kukusaidia kupata suluhisho la kile kinachokusumbua. Kumbuka, kuna watu ambao wanaweza kuwa wamepitia hali kama wewe. Hata hivyo, ikiwa haufikiri kuzungumza, unaweza kuandika hisia zako.
7. Epuka njia mbaya za kukabiliana na msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo kunaweza kusababisha kuongezeka kwa kishawishi cha kutumia madawa ya kulevya kama vile pombe, sigara, na vitu vingine. Ingawa dawa hizi zinaweza kusaidia kwa muda, husababisha hatari kubwa kiafya.
Matumizi mabaya ya dawa za kulevya pia husababisha ulevi, kuongezeka kwa viwango vya msongo wa mawazo na athari mbaya za kitabia na kijamii.
Jitahadhari na tabia zingine mbaya za kukabiliana na msongo wa mawazo kama vile kula sana na mazoea hatari ya uhusiano kama tabia hatari za kingono ambayo ni hatari kwa afya yako.
Tazama video hii kwa vidokezo zaidi kuhusu jinsi ya kukabiliana na msongo wa mawazo.
8. Tafuta huduma za ushauri wa kitaalam :
Unapaswa kutafuta msaada ikiwa una mawazo ya kujiumiza, kuhisi kuzidiwa, kuhisi kuwa huwezi kukabiliana au unatumia pombe na / au dawa za kulevya mara kwa mara kwa sababu ya msongo wa mawazo.
Huduma za ushauri zinatolewa bure kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi huko Kakuma, Dadaab na Nairobi.
Ikiwa wewe au mpendwa wako anahisi kuwa anahitaji kuongea na mtaalamu, tumia anwani zilizo hapa chini kupata usaidizi.
9. Tafuta huduma za ushauri wa kitaalam :
Unapaswa kutafuta msaada ikiwa una mawazo ya kujiumiza, kuhisi kuzidiwa, kuhisi kuwa huwezi kukabiliana au unatumia pombe na / au dawa za kulevya mara kwa mara kwa sababu ya msongo wa mawazo.
Huduma za ushauri zinatolewa bure kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi huko Kakuma, Dadaab na Nairobi.
Ikiwa wewe au mpendwa wako anahisi kuwa anahitaji kuongea na mtaalamu, tumia anwani zilizo hapa chini kupata usaidizi.
Nairobi
1. Center for Victims of Torture - 0790781359
2. Danish Refugee Council.
Unaweza kuwatembelea hapa katika ofisi zao zinazopatikana kwenye Kanisa ya PCEA Eastleigh Church ama uwapigie simu kwenye nambari ya bure 0800720309 ili kupanga mkutano.
3. Refugee Consortium of Kenya (RCK). Inapatikana Haki House, kwenye Barabara ya Ndemi. Kwa Mawasiliano:
• Msaada wa Ushauri: - 0716391412/ 0703820361
• Msaada wa Kesi za Dhuluma ya Kijinsia - 0740739386
4. RefuSHE Kenya-Inapatikana hapa.
6. Kituo cha Sheria. Inapatikana hapa - 0720806531
7. National Council of Churches of Kenya (NCCK) - 0704873342
Kakuma
1. AIC Health Ministries
AIC 0800720845
Nalemsekon Dispensary: 0702637769
Naregae Dispensary 0745330015
2. International Rescue Committee (IRC)
Kaapoka Health Centre (Main Hospital), Kakuma 1,
Lochangamor Dispensary/Clinic (Clinic 4), Kakuma 1
Hong-Kong Dispensary/Clinic (Clinic 2), Kakuma 2
Nationokor Dispensary/Clinic (Clinic 6), Kakuma 3
Ammusait General Hospital (IRC General Hospital), Kakuma 4
Wasiliana nao kwa nambari: 0792067135.
3. Danish Refugee Council (DRC):
Msaada kwa watoto, watu wazima na waathirika wa dhuluma za kijinsia katika Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma na Makazi ya Kalobeyei. Wasiliana nao kupitia nambari: 0800720414.
Dadaab
1. Kenya Red Cross Society (KRCS) – 0701494904
2. Hagadera refugee camp hospital (IRC)- 0704600513
3. Doctors Without Borders (MSF) Dagahaley - 0790205727
Iwapo una maswali yoyote, wasiliana nasi kupitia ukurasa wa Julisha.Info kwenye mtandao wa Facebook, kila Jumatatu hadi Jumamosi kutoka saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.