Ilani hii ya Kidakuzi ("Ilani") inafafanua jinsi Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji(International Rescue Committee) ("IRC") hutumia vidakuzi na teknolojia zingine za kufuatilia kupitia tovuti yetu ya Julisha.Info. Ilani hii itasomwa pamoja na ilani ya Faragha ya IRC, ambayo inaeleza jinsi IRC inavyotumia taarifa za kibinafsi. Ikiwa hukubali matumizi yetu ya vidakuzi, tafadhali zima kwa kufuata mwongozo wetu hapa chini.
Vidakuzi vya tovuti ni nini?
Vidakuzi vya wavuti ni faili ndogo ambazo huwekwa kwenye kompyuta yako au kifaa cha mkononi na tovuti unapoitembelea. Zina maelezo ya historia yako ya kuvinjari kwenye tovuti hiyo na kukutofautisha na watumiaji wengine. Vidakuzi hurejesha data kwa tovuti asili katika kila ziara inayofuata au kuruhusu tovuti nyingine kutambua kidakuzi. Vidakuzi ni muhimu kwa sababu huruhusu tovuti kutambua kifaa cha mtumiaji na, kwa mfano, kukumbuka mapendeleo yako na kwa ujumla kuboresha matumizi yako ya mtandaoni. Kama tovuti nyingi, tovuti za Julisha.Info hutumia vidakuzi.
Ingawa ilani hii inarejelea neno la jumla "kidakuzi", ambayo ndiyo njia kuu inayotumiwa na tovuti yetu kuhifadhi habari, nafasi ya hifadhi ya ndani ya kivinjari pia inatumika kwa madhumuni sawa na tunaweza kutumia teknolojia nyingine za ufuatiliaji kupitia tovuti hii kama vile vinara za wavuti. Kwa hivyo, maelezo yaliyojumuishwa katika ilani hii yanatumika vile vile kwa teknolojia zote za ufuatiliaji tunazotumia.
Unaweza kujua zaidi kuhusu vidakuzi katika www.allaboutcookies.org.
Mbona tunatumia vidakuzi?
- Ili kukuruhusu kufanya mambo kwenye tovuti yetu -- kwa mfano, vidakuzi hukuwezesha kuingia kwenye maeneo salama ya tovuti yetu, kujaza fomu za maombi au kutazama maudhui.
- Kukusanya takwimu zisizojulikana -- maelezo yanayokusanywa na vidakuzi hutuwezesha kuboresha tovuti kupitia takwimu za matumizi na ruwaza. Kwa mfano, ni muhimu sana kuona ni kurasa zipi za tovuti -- na kwa hivyo ni zipi kati ya huduma zetu -- ambazo ni maarufu zaidi na jinsi watumiaji wanavyowasiliana nazo. Pia hutusaidia kufahamisha ni maeneo gani tunahitaji kuboresha ufikiaji.
- Ili kuboresha matumizi yako ya tovuti yetu -- kwa mfano, ili kukuzuia kuingiza tena maelezo wakati tayari umefanya hivyo, au kwa kuhakikisha kwamba watumiaji wanaweza kupata kile wanachotafuta kwa urahisi.
- Ili kuhakikisha kuwa tovuti yetu ni salama -- kwa mfano, kuhakikisha kuwa taarifa za kibinafsi unazotupa hazianguki katika mikono isiyo sahihi.
- Ili kukupa taarifa na maudhui ambayo tunafikiri yanafaa kwako -- kwa mfano, kufanya kazi na washirika wetu ili kukuhudumia kwa utangazaji unaolengwa.
Jedwali hili linatoa habari zaidi kuhusu vidakuzi tunavyotumia na kwa nini.
Jina la Kidakuzi | Mtoaji | Kusudi la kidakuzi | Muda |
Google Analytics | Kuna vidakuzi hutumika kukusanya taarifa kuhusu jinsi wageni wanavyotumia tovuti zetu. Tunatumia maelezo kutayarisha ripoti na kutusaidia kuboresha tovuti. Vidakuzi hukusanya taarifa kwa njia isiyojulikana, ikijumuisha idadi ya wanaotembelea tovuti, ambapo wageni wametoka kwenye tovuti na kurasa walizotembelea. Bofya hapa kwa muhtasari wa faragha katika | Kikao chochote cha tovuti | |
Google Signals | Unapokubali vidakuzi, Google Analytics itahusisha maelezo ya kutembelewa ambayo inakusanya kutoka kwa tovuti na programu na maelezo ya Google kutoka kwa akaunti za watumiaji walioingia katika akaunti ambao wameidhinisha uhusiano huu kwa madhumuni ya kuweka mapendeleo ya matangazo. Maelezo haya ya Google yanaweza kujumuisha eneo la mtumiaji wa mwisho, na data ya demografia, na pia data kutoka kwa tovuti zinazoshirikiana na Google—na hutumiwa kutoa maarifa yaliyojumlishwa na yasiyotambulisha utambulisho wa tabia za watumiaji wa vifaa mbalimbali. | Kikao chochote cha tovuti |
Kukubalika kwa vidakuzi vya tovuti
Kwa kusoma kidokezo cha vidakuzi unapotembelea tovuti unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama vinavyosasishwa mara kwa mara. Hasa, unakubali vidakuzi kuhifadhiwa kwenye kompyuta yako na/au kifaa cha mkononi (isipokuwa kitakataliwa au kuzimwa na kivinjari chako).
Jinsi ya kuzima vidukizi
Vivinjari vya mtandao kwa kawaida hukubali vidakuzi kwa chaguo-msingi. Hata hivyo, vivinjari vingi hukuruhusu kuzima vidakuzi vyote au vya watu wengine(third-party cookies). Unachoweza kufanya inategemea kivinjari unachotumia. Ikiwa hukubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa hapo juu, tafadhali weka kivinjari chako kukataa vidakuzi, tembelea http://www.youronlinechoices.com/uk/ ili kujifunza zaidi kuhusu vidakuzi au kusakinisha kizima vidakuzi kama vile https:/ /www.ghostery.com/ optout.aboutads.info au http://optout.networkadvertising.org/. Hata hivyo, tafadhali fahamu kwamba kwa kutokubali matumizi yetu ya vidakuzi hii inaweza kuathiri au kupunguza uwezo wako wa kutumia tovuti yetu. Utendaji wa kufanya hivi kwa kawaida hupatikana katika chaguo, mipangilio au menyu ya mapendeleo ya kivinjari chako au kifaa cha mkononi.
Unaweza kuchagua kutoka kwa vidakuzi vya uchanganuzi vya Google kwa kutembelea ukurasa wa kujiondoa wa Google -https://tools.google.com/dlpage/gaoptout.
Bofya kwenye viungo vilivyo hapa chini ili kujua jinsi ya kubadilisha mipangilio ya kidakuzi chako katika:
Maelezo zaidi kuhusu utangazaji mtandaoni
Kampuni za utangazaji tunazofanya kazi nazo kwa ujumla hutumia vidakuzi na teknolojia sawa za kufuatilia kama sehemu ya huduma zao. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi watangazaji kwa ujumla hutumia vidakuzi na chaguo wanazotoa, na hatua unazoweza kuchukua ili kuchagua vidakuzi unavyoweza kukubali au kukataa, unaweza kukagua tovuti ya European Interactive Digital Alliance.
Kwa kuongeza, kuna programu inayokuwezesha kutumia mipangilio inayokuruhusu kuchagua vidakuzi vilivyowekwa kwenye kompyuta yako au kifaa cha mkononi, kama vile programu ya Ghostery.
kusasisha ilani hii
Tunaweza kusasisha matumizi yetu ya vidakuzi mara kwa mara na kwa hivyo tunaweza kusasisha Ilani hii. Kwa hivyo tunapendekeza uangalie Ilani hii mara kwa mara. Tutakuarifu kuhusu mabadiliko yoyote muhimu kupitia notisi kwenye tovuti yetu au kwa kuwasiliana nawe moja kwa moja inapowezekana.
Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820) ,Jumatatu hadi Ijumaa kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni