Dengue ni maambukizi ya virusi yanayoambukizwa kwa binadamu kupitia kuumwa na mbu walioambukizwa - hasa mbu wa Aedes Egypti, ambao hupatikana zaidi katika maeneo yenye joto. Kumekuwa na milipuko kadhaa ya homa ya Dengue nchini Kenya tangu kisa cha kwanza mnamo 1982. Kwa mfano, kulingana na ripoti ya Reliefweb, mnamo 2021, wakati wa mlipuko wa homa hii katika mkoa wa pwani wa Kenya, zaidi ya kesi 1,788 ziliripotiwa.

Ingawaje baadhi ya maambukizi huwa na dalili mbaya za mafua zinazohitaji uingiliaji wa matibabu, zaidi ya 80% ya maambukizi sio kali na hayaonyeshi dalili nyingi. Kutokana na hali hiyo, haijulikani kwa uhakika kumekuwa na visa vingapi vya homa ya hivyo, hawakuwahi kuripotiwa.

Dengue inazidi kuongezeka duniani kote, na karibu nusu ya watu duniani sasa wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kuna maambukizi ya homa ya dengue kati ya milioni 100 hadi milioni 400 kila mwaka.

 

Sababu/Maambukizi

  • Kuumwa na mbu wa Aedes

Homa ya Dengue huenezwa hasa kwa kuumwa na mbu wa Aedes walioambukizwa. Mbu huambukizwa pale anapomuuma mtu ambaye ana dengue katika damu yake. Baada ya wiki moja, mbu huyo anaweza kueneza ugonjwa huo kwa mtu mwingine wakati anauma. Mbu hawa hupatikana hasa katika maeneo yenye joto.

 

  • Njia nyingine ambazo homa ya Dengue inaweza kuenea

Maambukizi ya mama kwa mtoto- Kuna ushahidi wa uwezekano wa homa ya Dengue kupitishwa kutoka kwa mama mjamzito hadi kwa mtoto wake. Hii, hata hivyo, inahusishwa na muda wa maambukizi wakati wa ujauzito. Maambukizi wakati wa ujauzito yanaweza kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mdogo, mtoto kuzaliwa kabla wakati wake kufika au mtotokupata matatizo ya kiafya kabla au wakati wa uchungu wa kuzaa. 

Homa ya Dengue pia imegundulika kuenea kupitia uchangiaji wa viungo na kuongezewa damu, ingawa hizi ni kesi nadra sana.

Dengue haiwezi kusambazwa moja kwa moja kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Unajuaje ikiwa wewe au mtu mwingine ana homa ya Dengue?

Homa ya Dengue inaweza kuanza na joto kali ya mwili inayodudumu kwa siku 2-7. Mtu anaweza pia kuwa na:

• Kuumwa na kichwa sana

• Maumivu nyuma ya macho

• Maumivu ya misuli na viungo

• Kuhisi kichefuchefu- kuhisi kama kutapika 

•Kutapika

• Nyanda zilizovimba

• Majivu

  • Dalili mbaya zaidi ni pamoja na:

• Kuumwa na tumbo sana

• Kutapika kwa muda mrefu

• Kupumua kwa kasi

• Kutokwa na damu kwenye fizi ya meno au pua 

• Kuhisi uchovu sana

• Kutoweza kutulia

• Kufura kwa ini

• Damu katika matapishi au kwenye choo

 

Jinsi ya kugundua homa ya dengue

Daktari au mtoa huduma mwingine wa afya anaweza kushuku kuwa mgonjwa ana homa ya Dengue kulingana na dalili zinazoonekana, hasa ikiwa joto ya mwili inaambatana na dalili zingine mbili za Dengue. Historia yako ya kusafiri inaweza pia kudhibitisha.

 

 

Matibabu

Homa ya Dengue haina matibabu maalum. Mbali na kupumzika na kunywa maji mengi, matibabu ni kama vile matumizi dawa za uchungu kudhibiti maumivu na joto ya mwili. Mgonjwa akizidiwa anaweza ili kupewa huduma za matibabu kwa karibu.

Upatikanaji wa huduma  za matibabu zinazofaa ni muhimu kwa kuzuia maambukizi kuwa mabaya zaidi.

Kuzuia homa ya Dengue

Ulinzi dhidi ya kuumwa na mbu kwa kutumia:

  • Dawa za kuzuia mbu.
  • Neti za mbu.
  • Kuvaa nguo za mikono mirefu na suruali ndefu ili kuepuka kuumwa na mbu.

Kupunguza mbu katika mazingira:

• Kusafisha mazingira ambapo mbu huishi na kutaga mayai yake/kama vile vichaka na maji yaliyotulia.

• Utupaji sahihi wa taka za vyoo

• Kufunika, kutoa maji mara kwa mara kutoka vyombo vya kuwekea maji nje, na kuvisafisha kila wiki

• Kutumia viuatilifu (dawa za kuua wadudu) vinavyofaa kwenye vyombo hivi vya kuhifadhia maji.

 

Vituo vya Afya vya Kakuma

KITUO CHA AFYAMAHALIMAWASILIANO
Kaapoka Health Centre / Main HospitalKakuma 1Simu : 0715913104
Lochangamor Dispensary / Clinic 4Kakuma 1Simu :0712836854
Hong-Kong Dispensary / Clinic 2 Kakuma 1  Simu :254712837204
Nalemsekon Dispensary/ Clinic 5Kakuma 2Simu : 0712836854
Nationokor Dispensary / Clinic 6Kakuma 3Simu: 254712837055/
Ammusait General Hospital / Clinic 7Kakuma 4Simu 0712840214
Natukubenyo Health Center / Kalobeyei Health centreKalobeyei V1Simu: 0715913104
Naregae Dispensary/ Kalobeyei Village 2 ClinicKalobeyei V2 Simu: 0712837055  

 

  • Vituo vya Afya vya Daadab: 
KITUO CHA AFYAMAHALIMAWASILIANO
Red CrossIfo Camp -IFO Main Hospital, Health Post 7 & Health Post 1.

Simu: 0110483063

WhatsApp: 0110483063

MSF HospitalDagahaley Camp –MSF Main Hospital,Health Post 7 & Health Post 4 Simu: 0708 847905
Hagadera refugee camp hospitalHagadera refugee camp –IRC Main Hospital,Health Post E6 & Health Post L6.Simu: 0701629393

 

Maelezo ya huduma za afya yanaweza kupatikana kwenye ramani ya huduma ya Julisha.info:

https://www.julisha.info/sw/categories/1500000107582

 

Ili kufikia ramani ya huduma kwenye wavuti ya Julisha.info, bonyeza chaguo la "Service Map". Kutoka hapo, chagua mkoa wako, ambao unaweza kuwa Turkana, Garissa, au Kaunti za Nairobi. Baada ya kuchagua eneo lako, unaweza kupunguza zaidi utafutaji wako kwa kuchagua eneo lako maalum ili kufikia huduma zinazopatikana katika eneo hilo.

Kwa ufikiaji rahisi, unaweza pia kuchuja huduma unazohitaji kwa kubofya kitufe cha the "All services"kilicho upande wa juu kulia wa skrini yako. Hii itakuwezesha kuzingatia huduma maalum za afya unazohitaji.