Jambo la Kuzingatia: Mnamo Oktoba 2022, serikali ya Kenya iliteua jopokazi la kukusanya maoni ya umma kuhusu utekelezaji wa Mtaala unaozingatia Umahiri (CBC) na kutoa mapendekezo. Ukusanyaji wa maoni ya umma ulihitimishwa mnamo Novemba 2022. Kwa sasa serikali inapitia matokeo ya jopokazi hilo. Mara tu mchakato huu utakapokamilika, tutasasisha makala haya ili kujumuisha mabadiliko yatakayofanywa kwenye mtaala.

Mnamo Desemba 2017, Wizara ya Elimu ya Kenya ilizindua mfumo mpya wa elimu chini ya mtaala wa CBC (Competency Based Curriculum). Mtaala wa CBC ulichukua nafasi ya mfumo wa zamani. Awali, elimu ya msingi ilitolewa katika kipindi cha miaka 8, ikifuatiwa na miaka minne ya elimu ya sekondari na mingine minne ya elimu ya juu. CBC iliondoa  mfumo wa zamani (8-4-4) na sasa masomo ni kwa kipindi  cha miaka miwili, sita, mitatu na mitatu (2-6-3-3). CBC kwa sasa inatumika kufundisha na kutathmini wanafunzi nchini Kenya. 

Katika makala haya, Julisha.Info inafafanua yale unachohitaji kujua kuhusu elimu katika kiwango cha PP1 na PP2 katika mfumo wa  CBC nchini Kenya. Soma  ili kuelewa kile kinachohitajika ili kuwaandikisha watoto wako shuleni, na kile watakachojifunza katika miaka yao ya kwanza shuleni chini ya mtaala mpya. 

Wakenya au raia wa kigeni walio na cheti cha kuzaliwa cha Kenya, Kitambulisho cha mkimbizi  wanaweza kujiandikisha katika mfumo wa elimu wa Kenya. 

Ikiwa wewe ni mkimbizi au mtafuta hifadhi nchini Kenya, unaweza  kuwaandikisha watoto wako katika shule  kambini ikiwa una kadi ya mgao wa chakula (Ration Card) au, uthibitisho wa kujiandikisha (Manifest). Watoto wanaweza kujiunga na shule, kambini au sehemu zingine za nchi ikiwa unaishi nje ya kambi.  

Ikiwa huna hati zozote kati ya hizi, mtoto wako bado atakuwa na haki ya kuwa shuleni. Mkuu wa shule lazima afahamishwe kuhusu upotevu au ukosefu wa nyaraka zinazohitajika kabla ya kusajiliwa. 

Mtoto anapaswa kujiunga na PP1 wakati gani? 

Wazazi na walezi wanatarajiwa kuwaandikisha watoto wao shuleni mara tu wanapofikisha umri wa miaka minne. 

Ngazi ya kwanza ya elimu chini ya CBC, iko katika hatua mbili. Masomoya awali yamegawanywa katika viwango viwili: 

  • Hatua ya kwanza huitwa (Pre-primary 1 - PP1) na ni kwa watoto wa miaka nne. 
  • Hatua ya pili huitwa (Pre-primary 2- PP2) na nikwa watoto wa miaka tano. 

Masomo (pia yanajulikana kama malengo ya za kunza katika CBC) yanatolewa katika PP1 na PP2 ni: 

  • Lugha na mawasiliano 
  • Hisabati 
  •  Mazingira 
  • Kisaikolojia (kujifunza shughuli za kimwili) na ubunifu (muziki, sanaa na ufundi) 
  •  Dini. 

pre-primary_SWA.png

Ni lugha ipi inayotumika kufunza wanafunzi katika PP1 na PP2? 

Mafunzo katika shule ya awali na ya msingi hufanywa kwa kutumia lugha inayotumika katika eneo anakosoma mtoto.. Walimu pia wanashirikishwa kutoka eneo hilo ili kurahisisha kazi ya kuwafundisha watoto. 

Mafunzo huwezeshwa  na tafsiri ya mwalimu kwa lugha inayotumika katika eneo la shule. Katika maeneo ya watu wenye mchanganyiko wa lugha  au mijini, walimu hutumia Kiingereza na Kiswahili. 

Katika kiwango hiki, watoto hujifunza kueleza hisia zao, mawazo, na maoni yao kwa uwazi na kwa kujiamini na kwa lugha wanayoelewa. Aidha, wanafunzi watatayarishwa kujifunza jinsi ya kusoma na kuandika. Maagizo halisi ya kusoma na kuandika yapo chini   Grade 1, 2 na 3 kwenye mfumo wa  CBC. 

Nini cha kutarajia kutoka kwa mtoto baada ya kumaliza elimu yake ya PP1 na PP2 

  • Kupata stadi zinazofaa za mawasiliano, kama vile kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika.
  • Kuwa na ujuzi wa kimsingi wa kuchora na kutengeneza picha; kupaka rangi kusuka, kutengeneza maumbo, kutengeneza bangili, na kupamba.
  • Kuhesabu nambari (1-50), kipimo, na utambulisho wa sarafu ya Kenya, ruwaza
  • Ufahamu wa nyakati kwa kimsingi na taratibu za kila siku.
  • Kuzingatia usafi sahihi, usafi wa mazingira, na lishe (kunawa mikono, kuvaa, kusafisha pua, choo, kulisha).
  • Aonyeshe kuelewa  maadili ya kidini na maarifa ya kimsingi ya elimu ya dini ya Kikristo/Kiislam/Kihindu. Walimu wanatakiwa kuwasaidia wanafunzi kuthamini watu wa asili tofauti za kidini.

Je, wanafunzi watafanya mitihani katika ngazi za PP1 na PP2? 

Chini ya CBC, tathmini za elimu ya shule ya awali hufanywa kupitia maswali  , uchunguzi na hifadhi ya kumbukumbu za shughuli na mafanikio na ushiriki wa mtoto katika vigezo  vyote vya masomo. Uwezo wa wanafunzi shuleni yatatathminiwa na kulingana na vigezo vifuatavyo: 

  • Zaidi ya matarajio - Alama ya juu zaidi inayotolewa wakati mwanafunzi anapofanya vizuri au kukamilisha shughuli zote kama inavyotarajiwa.
  • Ameafikia matarajio - Mwanafunzi mwenye uwezo wa kufuata maelekezo kwa usahihi; anafanya kazi ipasavyo na kamilisha shughuli nyingi katika masomo.
  • Hajaweza kuafiki matarajio - Mwanafunzi anajaribu kufuata maelekezo lakini si kila mara na hajaweza kukamilisha baadhi ya mazoezi  au shughuli katika maeneo mbalimbali ya masomo
  • Chini ya matarajio - Pale ambapo mwanafunzi anaonekana kuwa na dosari kubwa au kutoweza kukamilisha kazi zozote kama alivyoelekezwa na mwalimu.

Vifaa  vinazohitajika katika kutoa mafunzo ya PP1 na PP2 chini ya CBC  

Wazazi na walezi wa watoto  katika kiwango cha PP1 na PP2 wanatakiwa kuwapatia wanafunzi vifaa  vinazopatikana kwa urahisi ili kukuza masomo na tathmini shuleni. Baadhi ya vifaa  hutolewa shuleni, navingine lazima vitolewe kwa nyumbani. Vifaa hivini kama: 

  • Mazingira ya asili, yaliyotengenezwa na mwanadamu 
  • Video na nyenzo za sauti za kidijitali
  • Vvitabu, mabango, Biblia ya Habari Njema
  • Vyombo vya hali ya hewa, picha na michoro
  • Majarida na magazeti
  • Chati, udongo, nyuzi
  • Vitambaa  vya nguo, vyombo
  • Vifaa vya kutumika chooni na vifaa vya usafi – unawaji mikono na vifaa vya kupigia mswaki• Maji, mwanga, vyanzo vya sauti - ngoma, vijiti, metali, shanga, manyoya

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820), Jumatatu hadi Jumamosi kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni