PIN ya KRA ni Nambari ya Utambulisho wa Kibinafsi inayotolewa na Mamlaka ya Mapato ya Kenya (Kenya Revenue Authority-KRA) kwa Wakenya au wakaaji wenye uraia wa nchi nzingine. KRA PIN ni muhimu kwa kufungua akaunti ya benki, kupata kazi na kufanya biashara nchini Kenya. 

Kulingana na mamlaka ya KRA, baadhi ya shughuli maarufu zinazohitaji PIN ya KRA ni pamoja na; 

  • Unapotuma ombi la kibali cha kufanya biashara (business permit) 
  • Usajili wa majina ya biashara na makampuni 
  • Utoaji leseni ya biashara - leseni ya biashara ni idhini rasmi ambayo utahitaji ili kufanya biashara. Leseni hizi mara hutolewa na serikali za kaunti. 
  • Ombi la usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (Value Added Tax - VAT) - chini ya sheria za Kenya, usajili wa VAT ni lazima kwa watu ambao wamesambaza au wanaotarajia kusambaza bidhaa zinazotozwa ushuru zenye thamani ya Kshs5,000,000 na zaidi ndani ya miezi 12. Unaweza kujifunza zaidihapa. 

KRA hutoa Nambari moja ya PIN kwa kila mtu pekee na inaweza tu kutumiwa na mtu ambaye ilitolewa kwake na haiwezi kutumiwa na wengine. 

Katika makala haya, Julisha.Info itukuongoza ili kujua jinsi ya kupata Nambari ya Pin ya KRA kama mkimbizi nchini Kenya. 

Jinsi ya kujiandikisha na kupata PIN ya KRA mtandaoni 

Ili kusajili na kupata PIN yako ya KRA kutoka kwa Mamlaka ya Mapato ya Kenya, tafadhali kumbuka kuwa unahitaji kuwa na Hati ya Utambulisho wa Mkimbizi (Kitambulisho) 

Ikiwa tayari una hati hii, fuata hatua zilizojadiwa hapa chini ili kujiandikisha kwa PIN yako ya KRA. 

  • Tembelea tovuti ya kujihudumia ya Mamlaka ya Mapato ya Kenya - KRA (iTax) kwa kubofya hapa.    
  • Teua - "New PIN Registration"  
  • Chagua "Non-Individual" na "Online Form" kama njia yako ya usajili na ubofye ‘next.’ 

blobid3.png

  • Jaza taarifa zako za msingi, na kisha chagua ‘Non-Kenyan Resident’ 
  • Chagua wajibu wa kodi unaofaa kwa kuteua masanduku husika. KUMBUKA: UsichaguesYES kwenye sehemu inayouliza iwapo unataka kujisajili kwa mfumo wa Turnover Tax  (TOT). Utahitaji tu kusema  YES  iwapo unahitimu mahitaji ya kulipa Turn Over Tax (TOT) kwa sababu mfumo huu hutumika tu kwa wakazi  wenye mapato zaidi ya Ksh1,000,000 (milioni moja) na haizidi wala kutarajiwa kuwa Zaidi ya Ksh50,000,000 (Millioni hamsini) kwa mwaka.  
  • Weka maelezo ya eneo lako la kazi au taaluma kutoka kwa chaguo zinazopatikana kwenye mfumo huu. Jaza Nambari yako ya Kitambulisho cha Mkimbizi, tarehe ya kuzaliwa, jinsia na nchi ya asili. 
  • Onyesha anwani yako ya mahali na anwani ya posta. Ongeza maelezo yako ya mawasiliano katika sehemu zilizotolewa. Kumbuka kuwa Anwani ya barua pepe (Email) na nambari ya simu ni lazima. 
  • Jaza maswali ya YES na NO chini ya maelezo yako ya mawasiliano na uambatishe nakala zilizochanganuliwa za Kitambulisho chako cha Mkimbizi. Nakala hizi ziwe zinazoonyesha pande zote mbili za kitambulisho chako. Hatua hii ni lazima.  

Baada ya kukamilisha hatua zilizo hapo juu, utapokea risiti ya uthibitisho ambayo utahitaji kuwasilisha katika ofisi za KRA,Times Tower mjini Nairobi, pamoja na hati zingine muhimu, ili kukamilisha mchakato wako wa usajili wa PIN ya KRA. 

Tafadhali kumbuka kuwa maombi yote ya PIN ya KRA ya wakimbizi yanaweza tu kukamilishwa katika ofisi za KRA zilizoko Times Tower jijini Nairobi kando ya barabara ya Haile Selassie. Ofisi zinafunguliwa siku za kazi kati ya 8:00 asubuhi na 5:00 jioni.  

Unaweza pia kuwasiliana na Kituo cha simu cha KRA kupitia nambari ya simu +254770631827. KRA pia inaweza kupatikana kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia Twitter na Facebook. 

Ukichagua kuwasiliana na KRA kwenye mitandao ya kijamii, kumbuka kujilinda mtandaoni! Kwa usalama wako, hupaswi kujumuisha nambari yako ya simu, barua pepe, PIN, kitambulisho au maelezo mengine ya kibinafsi katika chapisho wazi kwa umma. Badala yake, tuma ujumbe wa moja kwa moja maarufu kama Direct Message. 

blobid2.png

Je, ni hati gani zinazohitajika ili kukamilisha mchakato huo katika ofisi za KRA, Times Tower? 

Mchakato wa uthibitishaji katika ofisi za KRA, Times Tower ndiyo hatua ya mwisho ya kupata cheti chako cha PIN ya KRA. Katika ziara yako ya ofisi za KRA, utahitaji kubeba stakabadhi hizi: 

  • Kitambulisho halali cha Mkimbizi (Refugee ID) au Kadi ya Kigeni (Alien Card)  - Uhalali wa Refugee ID sasa ni miaka 5. 
  • Barua ya kukutambulisha kutoka kwa Refugee Affairs secretariat.(RAS). 
  • Barua kutoka kwa mwajiri wako ikiwa umeajiriwa. 
  • Cheti cha Usajili wa Biashara ikiwa unafanya biashara. Unaweza kujifunza jinsi ya kupata Cheti chako cha Usajili wa Biashara hapa.  
  • Kibali cha kufanya kazi kutoka kwa Idara ya Uhamiaji (Class M permit). Kibali cha Class M hutolewa kwa mtu ambaye amepewa hadhi ya ukimbizi nchini Kenya kwa mujibu wa sheria ya mkimbizi ya Kenya na mwenzi yeyote wa mkimbizi kama huyo ambaye ana nia ya kuajiriwa au kujihusisha na kazi mahususi, biashara, biashara au taaluma. 
  • Stakabadhi ya kupokea ombi la PIN ya KRA iliyopokelewa mwishoni mwa mchakato eleza mapema katika makala haya..  

Baada ya kuwasilisha hati hizi, maafisa wa KRA watakuthibitisha na kukupa cheti cha PIN ya KRA kilichobeba maelezo ya kitambulisho chako na anwani ya mahali kama ilivyotolewa katika ombi lako. 

 

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie ujumbe wako kupitia ukurasa wetu wa  Facebook , Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.